USIOGOPE | Bible & Mission Centre
Katika Yeremia 29:11 Biblia inasema, Mungu anatuwazia mawazo ya AMANI na sio mawazo mabaya....lakini siku zetu za mwisho anasema atatupa TUMAINI. Lakini pamoja na ahadi hii kubwa ya Mungu, bado tumefika mahali sisi watoto wake KUOGOPA katika maisha yetu.
Wakati mwingine tunapitia katika vipindi vigumu ambayo vinatufanya tuwe na hofu, tuiname na kutokuwa na tumaini.
Lakini Bwana anasema, yeye anatuwazia mawazo yaliyo mema, kutupa tumaini nyakati zetu za mwisho.

Wewe si wa kwanza kupitia katika kipindi kigumu, wapo waliopita kama wewe, wengine walikuwa wafalme na wengine walikuwa manabii wa Mungu. Baadhi yao ni hawa wafuatao:-
NABII ELIYA
1Wafalme 19:2,3
Yezebeli alituma ujumbe kwake wa kumuua baada ya Eliya kuwauwa manabii 450 wa baali. Mstari wa tatu (3) katika tafsiri ya Kiswahili haionyeshi wazi kama Eliya aliogopa, lakini ukisoma tafsri ya Kiingereza inasema Eliya aliogopa na si tu kwamba "aliondoka" bali "alikimbia" ili kuiokoa roho yake.
Unaweza kuona vile tunaweza kuingiwa na hofu hata baada ya kuwa umetoka kufanya kazi kubwa na ya kijasiri kama ya Eliya ya kuwaua manabii wa Baali 450 lakini alipopata ujumbe huu wa yeye kuuwawa aliogopa na kukimbia.

MFALME DAUDI
1Samuel 26:1
Daudi alikuwa akiwindwa na Sauli naye alihofu akakimbia akajificha mapangoni. Lakini katika
yote hayo Mungu alimwokoa na mkono wa Sauli.

MTUME PETRO
Mathayo 14: 26-28
Wanafunzi wa Yesu waliogopa walipomwona Yesu anatembea juu ya maji wakidhaini ni mzimu. Yesu alipowaambia MSIOGOPE ni mimi Petro alipata ujasiri wa kumwambia Yesu amuamuru atembee juu ya maji, Yesu akamwambia Petro njoo....Petro akatoka chomboni akaanza kutumbea juu ya maji!! Lakini pamoja na kutembea juu ya maji kwa amri ya Yesu, bado Petro kwa kuangalia mazingira ya bahari yenye mawimbi, upepo nk, na kwa hofu hiyo akaanza kuzama.

Mpendwa na rafiki, ni nini leo katika maisha yako kinachokufanya UOGOPE na hata kutoa TUMAINI lako kwa MUNGU?
▪Je, ni hofu ya kifo pengine kwa sababu ya ugonjwa unaokutesa kwa muda mrefu?
▪Je, ni hofu ya karo ya watoto shule, kodi ya nyumba, biashara haiendi na bills nyingine nyingi?
▪Je, hofu yako ni maisha magumu na hata hujui leo yako itaisha vipi?
▪Je, ni hofu ya kutengwa au kukataliwa na wazazi ama ndugu, pengine kwa kwasababu umeokoka?
▪Je, ni hofu ya kukosa ajira, umesoma lkn huna kazi au una kazi isiyolingana na elimu yako?
▪Je, ni hofu ya maadui wanaokuwinda kwasababu umebarikiwa na pengine bila sababu yoyote?
▪Je, ni hofu ya maadui wa watoto wako?
▪Je, ni hofu ktk ndoa yako kwasababu hujapata mtoto na maneno ya kejeli kwako yamekuwa mengi?
▪Je, ni hofu kwasababu hujaoa au hujaolewa, na kila unayemgusa kuchumbia/kuchumbiwa anakukejeli au kukutupa? Una hofu utachelewa kuolewa au utachelewa kuoa?

USIOGOPE! USIOGOPE! USIOGOPE!
Isaya 41:13, Bwana anatupa neno la tumaini. Yeye anasema atakushika kwa mkono wake wa kuume na kukuokoa. Anasema USIOGOPE.
Mwanzo 26:24, Usiogope.
Kaza mwendo, endelea kumpenda kwakuwa yeye ni mpaji wa watu wote. Yeye ameahidi kutubariki na kuzidisha uzao wetu. Endelea kumpenda Mungu kwa kuwa yeye ameahidi kubariki uzao wetu.

2 Wafalme 6:16
Maadui wanaokuwinda ni cha mtoto kulinganisha na walio upande wetu. Na ni wengi na wana nguvu sana kuliko walio upande wa adui.
Bwana anaweza hata kukuandalia chakula machoni pa watesi wako na wakabaki wanashangaa ulinzi wa Mungu maishani mwako.

Kutoka 23:25-26
Naipenda mistari hii......Bwana anasema, "Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula cheko, na maji yako, nami nitakuondolea ugonjwa kati yako. Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza."

Mpendwa, wewe mtumikie Bwana na kesho yako ni bora kuliko jana kwa sababu Bwana anasema na wewe leo USIOGOPE na hata ni hofu ya kifo yeye amesema hesabu ya siku zako ataitimiza na kama ni utasa....amesema kwako hakutakuwa na atakayekuwa tasa wala kuharibu mimba na ataondoa kwako magonjwa kwako.
USIOGOPE KWA MAANA BWANA MUNGU YU PAMOJA NAWE!
Mungu akubariki sana,
Pastor, David Vincent.
Pastor, David Vincent.

Ahsante
ReplyDelete