Je! UMEANGUKA NA KURUDI NYUMA?? | Bible & Mission Centre
Ndugu yangu yamkini ulikuwa umesimama vyema katika wokovu na kuyatenda yale yampendezayo Mungu ila ghafla ukajikuta umerudi nyuma na kuanguka dhambini, ndugu yangu napenda kukuambia NEEMA bado ipo, unaweza kurudi na Bwana akakakupokea tena!!!
Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena,Mithali 24:16a Hata kama unaona umetenda dhambi ambayo unaona siyo rahisi kusamehewa,bado ipo nafasi ya KUTUBU (toba ya kweli ya kumaanisha kujuta) na ukasamehewa,usiogope! Hata kama watu watakucheka na kukunenea vibaya nakwambia Yesu anakupenda, rudi na kutubu ulipoanguka yeye ni Mungu wa rehema na neema,mvumilivu mwingi wa fadhili na kweli, anakusubiri rudi tu utasamehewa kwani Mungu ana upendo mwingi na utusamehe makosa yetu.
Yohana 6:37 "Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe" unaweza ukaona ni jinsi gani Yesu alivyo na upendo mwingi kwa kila aamuaye kugeuka na kumfuata, Katika Ezekieli 18:23 Neno la Mungu linasema "Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake akaishi?" Hapa ni dhahiri kabisa unaona Mungu mwenyewe anavyosikitishwa na kifo cha mtu mwovu lakini kwa vile bado anakupenda asema "Si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake akaishi? OOH HUU NI UPENDO WA AJABU SANA!
Nakusihi kwa Roho wa Bwana rudi rudi,rudi tena maana NEEMA YA MUNGU JUU YAKO BADO IPO !!
Bwana anakusubiri kumbuka hadithi ya mwana mpotevu ili ikutie moyo.
LIKE | COMMENT | SHARE na rafiki zako ili uwatie moyo wamrudie Bwana naa Mungu atakubariki.

No comments