SIFA NA KUABUDU HUVUTIA UWEPO WA MUNGU - SEHEMU YA II | Bible & Mission Centre
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo mpendwa msomaji.
Leo napenda kuchukua nafasi hii kumalizia kwa ufupi somo letu kama linavyoonyesha japo juu.
Wiki iliyopita nilimalizia kwa kusoma kitabu cha 2 Nya 5:13,14 (Soma tena..)

Leo nianze kwa kusema, Tunapomsifu na kumwabudu Mungu kuna nguvu kubwa sana ambayo haiwezi kutamkwa au kufikirika.
Hapa tunaweza kumjua Mungu vema zaidi, lakini pia hapa ni mahali penye ufunguo katika kumjua Yesu pia.
Tunapomsifu Mungu ni vema sana kulenga sifa zinazomhusu Mungu moja kwa moja, kumsema yeye kwa uzuri alionao na katika kutambua yale aliyoyafanya, anayofanya na atakayoyafanya. Lakini pia ni kutambua ukuu, enzi, mamlaka na ufalme wake usiotikisika.
Tukifanya kwa ubora na katika usafi wa mioyo, sifa na kuabudu ni kanuni ya kumvutia Mungu kushuka na kuanza kushughulika na maisha yetu binafsi.
Katika makusanyiko yetu tusiifanye ibada hii kuwa tu sehemu ya kumkaribisha muhubiri kuhubiri au kufanya tu kwa sababu iko kwenye ratiba na mpango wa ibada zetu.....bali hapa pawe ni sehemu ya kupeleka marhamu mazuri yanayonukia safi mbele za Mungu na kumvutia kushuka katika wingu la utukufu wake.

Sifa ni kiti cha enzi cha Mungu.... (Zaburi 22:3) "Na wewe u Mtakatifu, Uketiye juu ya sifa za Israel." Hebu fikiria tu kwa dakika moja, kwamba Mungu anakalia sifa!? Sijui wewe, lakini kwangu inanihamasisha kuyafanya maisha yangu yawe sifa kwa Mungu kila asubuhi, mchana na usiku, Mungu akalie sifa zangu.
Kwa hiyo tunahitaji kumsifu Mungu kwa uzuri wa utakatifu ili kumfanya Mungu kuzikalia sifa zetu na ninakuhakikishia hatutabaki kama tulivyo.

Kuabudu kunakovutia uwepo wangu ni lile tendo la kwenda mbali zaidi na kuingia katika kina zaidi cha urafiki na Bwana Mungu. (Intimacy)
Ni tendo la kuonyesha thamani ya hali ya juu kwa Mungu wako, na hapo ndipo mahali tunafika na kusema "Bwana sina mwingine kama wewe, wewe tu unanitosha, wewe tu ni furaha yangu....na zaidi na zaidi!" (Habakuki 3:17,18) Hata kama maisha hayako vile ulitaka yawe, bado THAMANI yako inapaswa kuwa MUNGU na kumwabudu yeye siku zote. Kwenye maisha yako usiweke mbele kazi yako, familia, mke, mume au watoto, bali muweke mbele MUNGU na kuwa thamani yako na hapo ndipo ibada yako itavutia uwepo wa Mungu naye ataanza kushughulika na maisha yako kuanzia ndani kuja nje. Utaponywa, utasamehewa, utanong'onezwa siri, utakuwa karibu zaidi naye, utazidi kufanana naye, utabadilishwa na kuwa mtu wa furaha daima.

No comments