SIFA NA KUABUDU HUVUTIA UWEPO WA MUNGU - SEHEMU YA I | Bible & Mission Centre
Kabla sijaendelea na fundisho langu leo, nichukue nafasi hii kukukaribisha katika blog yetu hii ambayo itakuwa inakuletea mafundisho ya neno la Mungu ambayo yatakufanya ukue na kukomaa kiroho.
Mpendwa msomaji, Sifa na Kuabudu ndio moyo wa Mungu mwenyewe mbinguni. Na inapaswa kuwa hivyo hapa duniani na hata chini ya nchi. Na kwa sababu hiyo kwetu, Bible & Mission Centre; Sifa na Kuabudu ndio kiini na kitovu cha ibada zetu kwa sababu Mungu anatafuta watu wa namna hii katika kizazi hiki sasa (Yn 4:23,24). Hii ndiyo sababu tumeona vema kukushirikisha umuhimu huu kwa njia ya mafundisho ili uwe miongoni mwa hao ambao Mungu anawatafuta wamwabudu.
Sasa karibu tuendelee…..
Uwepo wa Mungu katika maisha yetu, pengine ndio jambo muhimu tunalohitaji kuliko kitu kingine chochote. Kuwa na uwepo wa Mungu maishani mwetu ni kuwa na Mungu mwenyewe maishani mwetu.
Adam na Hawa walikuwa na ushirikiano wa karibu sana katika uwepo wa Mungu halisi (physical) kabla ya anguko. (Mwa 3:8) “Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adam na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone.”
Hii inatuonesha kuwa, Mungu alikuwa na kawaida ya kuwatembelea Adam na Hawa kila jioni na kuwa na wakati mzuri nao. Lakini dhambi ilipoingia ikawa kizuizi cha sisi kuwa na uwezo wa kuwa katika uwepo wa Mungu kwa uhalisia (physical). (Kut 33:20) “ Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.” Ni malaika watakatifu, wasio na dhambi ndio walio katika uwepo wa Mungu kiuhalisia. (Lk 1:19) “ Malaika akamjibu akamwambia, Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele za Mungu; nami nimetumwa niseme nawe, na kukupasha habari hizi njema.”

Ashukuriwe Mungu kwa wokovu wake kwetu. Kwa sababu leo wakristo tunaweza kuwa na uwepo wa Mungu ndani yetu. Huu ni uwepo tunaoupata mara tu baada ya kumwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wetu kwa njia ya ROHO MT. akaaye ndani yetu. (Yn 14:23) “Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.”
Mbali na uwepo huu ambao tunaupata kwa njia ya kumwamini Bwana Yesu Kristo, hapa napenda kuzungumzia uwepo ule unaovutwa na SIFA NA KUABUDU. Huu ni uwepo unaokuwa na udhihirisho wa Mungu. Ni uwepo maalum ambao ndani yake unakuwa na mambo yafuatayo:-
Ili kuingia na kufika katika kilele cha uwepo huu ni lazima Kanisa na wale wanaotuongoza kumwabudu Mungu kuwa na matarajio haya na kujua bila shaka yoyote nguvu iliyo nyuma ya kusifu na kuabudu.
Uwepo huu wa Mungu utatiririka katika mkutano na ibada na kuanza kugusa maisha ya watu, kuponya walio wagonjwa hata bila kuwekewa mikono, kuwafungua wengi kutoka nguvu za adui, kurejeshewa vyote vilivyoibwa na adui, kuingia katika ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi na kazi nyingine nyingi katika uwepo huu. (2 Nya 5:13,14) “hata ikawa, wenye panda na waimbaji walipokuwa kama mmoja, wakisikizisha sauti moja ya kumsifu na kumshukuru BWANA; nao wakipaza sauti pamoja na panda na matoazi na vinanda, wakimsifu BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele; ndipo nyumba ikajawa na wingu, naam, nyumba ya BWANA, hata makuhani hawakuweza kusimama ili kufanya huduma yao kwa sababu ya lile wingu; kwa kuwa nyumba ya Mungu imejaa utukufu wa BWANA.”
- UPAKO MAALUM
- KAZI MAALUM

Huu ndio ukweli tunaoupata katika neno la Mungu, kwamba tunapomsifu na kumwabudu yeye ni vema sana kufika katika uzoefu huu wa kuona wingu (uwepo - upako maalum) unashuka toka juu ili kuijaza nyumba ya Bwana na utukufu (kazi maalum) ukianza kudhihirika katika maisha ya watu, na watu wa Mungu wakiburudishwa katika uwepo huo.
Somo litaendelea wiki ijayo:
Pastor, David Vincent.

Ahsante sana Mchungaji kwa somo hili. Namshukuru Mungu kwa ajili yako, kukupaka mafuta kutufundisha kwa habari ya Kusifu na Kuabudu.
ReplyDeleteHabari hii itaenea kwa mataifa yote hata tuona mwili wa Kristo unajengwana kukomaa ili kufaa kwa Kazi hii maalum ya Kumwabudu Mungu wetu.