LATEST UPDATES:

Je wajua ni kwanini BMC tumeunda forum? | Bible &Mission Centre

bible and mission centre
Bwana Yesu asifiwe!
Nawasalimu sana katika Jina la Yesu.
Of course neno forum sio kitu kugeni yawezekana umewahi kulisikia neno hili mara kadhaa ila Bible and Mission Centre leo tarehe 31.08.2017 tumeanzisha forum ya awali kwa udhamini wa NABBLE forum ambayo ni ya kujadili kuhusu wokovu na kujibu hoja mbalimbali zinazomlenga Yesu moja kwa moja. Forum yetu inaitwa BMCforum.

Dhumuni hasa na dhamira kuu ya kuwa na forum hii:
1. Kuwaleta wateule wa Kristo pamoja na kujadili changamoto wanazokutanana nazo kwenye wokovu huu ambao ni kwa neema tu tunao na namna ya kuzikabili ili tuweze kuendelea na kudumu katika wokovu.
2. Jamii tuliyonayo sasa ni ya kuHoji (kuuliza) hasa pale tunapoipelekea habari njema za mwokozi wetu Yesu Kristo, Hivyo basi kwa jinsi hiyo forum hii BMCforum imetoa fursa kwa mtu wa dini yoyote kuHoji kuhusu Yesu tunae mwamini na atapata majibu yaliyo thabiti maana Bible and Mission Centre sisi hatuna wala sio dini bali sisi tunasimama Kulitukuza na Kuliadhimisha Jina la Yesu katika ROHO na KWELI.
3. Hatuwezi kumshinda shetani endapo hatuzijui mbinu zake, kupitia forum hii unaweza ukazifaahamu kwa namna moja au nyingine mbinu ambazo ibilisi anazitumia kuuwinda wokovu ulio nao.

Kujiunga Bofya hapa.

Kwa kujiunga kwako kama umeokoka itakuwa ni fursa pia ya kutumika kujibu hoja ambazo zitatolewa lakini pia kama hujapata neema ya kuokoka karibu ujifunze na kisha ufanye maamuzi mazuri maana Yesu yupo kwa ajili yako leo.

Ubarikiwe wewe unaesoma ujumbe huu cha muhimu usisahau kushare na rafiki zako katika mitandao ya kijamii, Na Mungu wa Mbinguni Akubariki.

Imetolewa na: Bible & Mission Centre
Kwa shida yoyote ya kimtandao kuhusu forum hii piga: +255626094600



No comments